KWANINI VIJANA WENGI HUKATA TAMAA MAPEMA?

Ujana ni umri uliojawa na mambo mengi kwa binadamu, na mambo hayo hua na athari kubwa kwa maisha yote ya mwanadamu husika. Hiyo ni kwakua katika umri huo ndipo maamuzi mengi yanayoamua hatima ya maisha hufanyika. Iwapo maamuzi sahihi hufanyika, basi huongeza nafasi ya mtu kufanikiwa kimaisha. Lakini iwapo maamuzi mabaya hufanyika, hupunguza uwezekano wa mtu kufanikiwa kimaisha.
Ikumbukwe pia umri huu huandamwa na changamoto nyingi sana, ikiwemo uhaba wa fedha, ushawishi wa marafiki, msukumo wa ukuaji, tamaa na mengineyo. Yote haya huhitaji uwezo wa mtu kuyamudu ili kupunguza uwezekano wa kuathirika nayo na kuongeza uwezekano wa kuyatumia kujifaidisha binafsi. Changamoto hizi na nyinginezo nyingi hupelekea mtu kushindwa kufikia malengo yake mapema, hivyo kuweza kudhani hatoyafikia. 
Hata hivyo kuna mambo ambayo ndiyo yanaonekana kukatisha tamaa vijana zaidi katika mihangaiko yao ya kimaisha. Machache ni kama yafuatayo;

1. Presha ya Umri

Vijana wengi wamekua wakikata tamaa kimaisha pale ambapo wanahisi tayari wamekua na umri unaotosha kujitegemea ama kua na maisha mazuri lakini bado hawajafanikiwa. Hii hufanya vijana wengi kuhisi kwamba hawana bahati kimaisha ama njia wanazotumia kujitafutia kipato sio nzuri. Fikra hizi huweza kupelekea ushawishi wa mtu kujihusisha katika shughuli za uhalifu, hata kuharibu kabisa kesho yake kwa matamanio ya kufanikiwa haraka katika umri flani.
Lakini sio kweli kwamba kufanikiwa ni swala la umri. Binadamu anakubwa na hali tofauti ambazo zinaweza kumfanya afanikiwe mapema kabla anavyofikiria, ama kuchelewa kufanikiwa kama anavyopanga, ama kufanikiwa katika muda aliopanga kufanikiwa. Mambo kama uwepo wa fursa katika mazingira, uwezo wa familia, uwepo wa mitaji, bahati na jitihada, vyote vina nafasi katika kufanikiwa.
Ni vyema kila mmoja kujiangalia mazingira yake na kutambua uwezekano wa kufanikiwa pasipo kuzingatia sana katika umri alio nao.

2. Kujilinganisha wa Watu Wengine

Swala jingine linaloumiza vijana wengi ni hali ya kujilinganisha na watu wengine, kama kipimo cha kufanikiwa. Hali hii hutokea pale ambapo mtu huhisi wenzake wa karibu wamefanikiwa kumzidi yeye, hata kupelekea kuhisi kwamba huenda kuna mahala anakosea. 
Ikumbukwe kila mmoja anatoka katika familia tofauti, ana uwezo tofauti, akili tofauti, mitizamo tofauti na hata maamuzi tofauti. Kujilinganisha na mtu mwingine sio sahihi sababu huenda yeye mazingira yake yamemuwezesha kufanikiwa mapema kabla yako, ama yamemchelewesha kufanikiwa.
Ni vyema kila mmoja kutizamana mafanikio yake kama swala binafsi, kuepuka kujilinganisha na wengine, na kuongeza jitihada kama njia ya kuweza kufanikiwa zaidi, bila kuzingatia wenzake wamefika mbali ama karibu kiasi gani kimafanikio.

3. Presha ya 'Deadline'

Swala jingine linalokwamisha vijana wengi katika kuendeleza jitihada zao kimaisha, ni kujiwekea vikomo vya muda katika kukamilisha jambo fulani. Vikomo hivyo hufanya mtu kuhisi amefeli kufikia malengo, hata kama amejitahidi kufika hapo halipo. Mfano mtu anaweza kupanga kuwa na nyumba yake afikishapo miaka 30. Kushindwa kua na nyumba baada ya umri huo kunaweza kumkatisha tamaa mtu huyo na kuhisi amefeli, hata kama amefanya mambo mengine ya kimaendeleo ikiwemo kukaribia kufikia lengo hilo.
Sio mbaya kujiwekea makadirio ya muda katika kufikia swala fulani, ila ni vyema kubadilisha makadirio hayo kutokana na sababu muhimu zinazoweza kuathiri ufikikaji wa malengo hayo. Hii itasaidia mtu kupata moyo zaidi kwa kile alichofanikiwa kukifanya, ukizingatia vikwazo ambavyo vinaweza kuwa vimemkwamisha kufika hapo.
Ahsante!
Wasiliana nami kwa Namba: +255 744 015 186

Comments

  1. Kazi nzuri sana Yahya Mafula, kundi kubwa la vijana litajifunza kupitia hi,, ningeomba kuwe na muendelezo ili vijana wengi waweze kujitambua na kufika malengo yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika ntaendelea kufanya tafiti niandike mengi. Ila vijana wengi hawapendi kusoma. Jitahidi pia kwenye nyimbo zako uwaelimishe zaidi. Sababu wanapenda muziki

      Delete
    2. Sawabroh! Sema muziki wenyewe sikuhizi mambo yame badilika, vijana wengi hawasikilizi nyimbo zenye ujumbe wa kuelimisha.

      Delete
    3. Usikatishwe tamaa na hao, hata kama ni wengi, lenga wachache watakaonufaika

      Delete
  2. Replies
    1. Ahsante kaka. Tuendelee kuelimisha jamii kadri tunavyoweza

      Delete
  3. Kaka Umetisha kweli, Ni Makala yenye ujumbe mzuri Sana wenye kufundisha na kuelimisha, sisi Kama vijana Kuna Mambo mengi Sana ya kujifunza ili tuweze timiza ndoto zetu✊🏿

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakika ndugu yangu. Ushindi wa Kijana mmoja ni ushindi wa vijana wengi wengine. Tutiane moyo kufika pale tunapopatamani

      Delete
  4. Kaka kwa hili hongera sana, tutajifunza mengi kukiwa na muendelezo wa chapisho nyingi, usikate tamaa pia kama fundisho hili ulilolitoa. Mungu atakubariki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana Ndugu yangu. Umenitia moyo katika hili na ntaendelea kufanya hivo. Hakika nguvu ya kijana ni vijana wenzake

      Delete
  5. Nimeipenda hii makala, asante kwa kukumbsha vjana, hii ni elimu njema sana, Big Up Bro

    ReplyDelete
  6. Ahsante sana Ndugu yangu. Tuendelee ku-supportiana kwenye mihangaiko yetu, tutafika tuu

    ReplyDelete
  7. Kwanza hongeraa Sana kwa kutufikishia ujumbe huu. Umejaribu kuwa muwazi Sana katika suala la namna ya kuyafikia mafanikio lakini pia sababu zinazo pelekea utofauti katika mafanikio mbali na umri, nafikiria hapa inawezekana kukawa na sababu nyingi zaidi lkn kwakuwa umeahidi kuwa patakuwa na muendelezo wa machapisho mengini inawezekana huko ndo tukajifunza zaidi. Ni Imani yangu kwamba hilo chapisho litakuja na majibu mazuri. Ubarikiwe.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante sana Ndugu yangu. Lakini pia mawazo yako ni ya msingi sana na nna imani yatatufunza mengine. Tuongezee tuu maarifa kaka

      Delete
  8. Bro xjawai kukuping kaka nakubali kwa kazi nzuri

    ReplyDelete
  9. dogo nazani huu ni mwanzo mzuri sana, keep it up @Epson

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ahsante Ndugu yangu Epson. Nawe unakaribishwa kuleta makala yako hapa tuichapishe kaka

      Delete

Post a Comment

Popular posts from this blog

UMUHIMU WA RASILIMALI WATU