Posts

Showing posts from January, 2020

UMUHIMU WA RASILIMALI WATU

UMUHIMU WA RASILIMALI WATU Na: YAHYA JUMA MAFULA Singida, Tanzania. Watu ni rasilimali muhimu kwa ukuaji wa taasisi na taifa lote kwa ujumla. Kuwa na rasilimali fedha, rasilimali ngumu, rasilimali asili, rasilimali teknolojia ama rasilimali muda pekee hakuwezi kuleta maendeleo yanayotarajiwa pasipokua na rasilimali watu. Rasilimali watu ndio hutumia rasilimali nyingine kuwezesha ufikiaji wa malengo. Kwa lugha nyingine rasilimali watu huitwa wafanyakazi ama watumishi. Rasilimali watu ni nini? Hawa ni watu wanaofanya kazi kwa mwajiri husika, kwa makubaliano ya kulipwa ujira kwa jitihada zao katika kutimiza malengo ya kundi, taasisi ama taifa. Aina za Rasilimali watu Aina za wafanyakazi hutegemena na mikataba husika ambayo hao wafanyakazi huajiriwa nayo. Mikataba ya wafanyakazi hao ni kama ifuatavyo; (a) Wafanyakazi wa mikataba ya kudumu Hawa ni wafanyakazi wanaoajiriwa kwa masharti ya moja kwa moja, kwamba wataitumikia taasisi mpaka watakapofikia umri wao wa kustaa...