Posts

Showing posts from October, 2021

KWANINI VIJANA WENGI HUKATA TAMAA MAPEMA?

Ujana ni umri uliojawa na mambo mengi kwa binadamu, na mambo hayo hua na athari kubwa kwa maisha yote ya mwanadamu husika. Hiyo ni kwakua katika umri huo ndipo maamuzi mengi yanayoamua hatima ya maisha hufanyika. Iwapo maamuzi sahihi hufanyika, basi huongeza nafasi ya mtu kufanikiwa kimaisha. Lakini iwapo maamuzi mabaya hufanyika, hupunguza uwezekano wa mtu kufanikiwa kimaisha. Ikumbukwe pia umri huu huandamwa na changamoto nyingi sana, ikiwemo uhaba wa fedha, ushawishi wa marafiki, msukumo wa ukuaji, tamaa na mengineyo. Yote haya huhitaji uwezo wa mtu kuyamudu ili kupunguza uwezekano wa kuathirika nayo na kuongeza uwezekano wa kuyatumia kujifaidisha binafsi. Changamoto hizi na nyinginezo nyingi hupelekea mtu kushindwa kufikia malengo yake mapema, hivyo kuweza kudhani hatoyafikia.  Hata hivyo kuna mambo ambayo ndiyo yanaonekana kukatisha tamaa vijana zaidi katika mihangaiko yao ya kimaisha. Machache ni kama yafuatayo; 1. Presha ya Umri Vijana wengi wamekua wakikata tamaa kimaisha p...